Picbear logo Browse Instagram content with Picbear

@nikkwapili

nikkwapili

nikkwapili

Msanii wa muziki wa hiphop, mwanazuoni,mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya weusi, pamoja na taasis ya maendeleo ya jamiii (www.twaonekana.org)

 • 252K Total Likes
 • 4K Tot. Comments
NDIO AU HAPANA (YES or No) maneno ya kawaida kabisa lakini yana madhara makubwa katika maisha yetu............watu wanatumia hapana au No mara nyingi, yani wagumu kushawishika wana nafasi ya kufanikiwa zaidi, kulipwa mshahara mkubwa, kuheshimika, kuuza bidhaa kwa bei nzuri, kupanda ngazi, kupendwa zaidi au ku hongwa zaidi........................kwa sababu No au hapana inaonesha unajiamini, una msimamo, unathamani, unajua, una mawazo binasfi .................watu wenye yesi nyingi au ndio.....watalipwa kidogo, watabaki chini, havutii zaidi, watapata thamani ndogo............................. Kwasababu ndio nyingi au yes nyingi zinaonesha udhaifu, urahisi kushawishika, kufuata upepo, kutokuwa na mawazo binafsi Ji tafakari je wewe ni mtu wa yesi/ndio nyingii na hapana chache au ni mtu wa hapana nyingi na ndio chache?????
Genius .......Link kwa bio yangu
LINK KWA BIO YANGU WEUSI + BELLA
Natamani nami nijuee.......utatunzaaa penziiii languuuuu LINK KWA BIO YANGU RAHA JIPE MWENYEWE SASA
Mchepuko vs (mke,mpenzi, mchumba wa kudumu) Katika ubongo wa mwanaume mke wake au mpenzi wa kudumu ana taswira nyingi ni mpenzi, mzazi mwenza, mtu wa kupanga nae maisha, ndugu zake ni ndugu zako, pia mlinzi wa tabia zako, kwa hiyo kisaikolojia unamwona katika taswira nyingi Lakini mchepuko unamwona katika taswira moja tu (tendo), hivyo atakua anakuvutia zaidi kwakua ni taswira moja tu, ubongo unakuwa focused Ndio mana wanaume wengi wanapowaza tendo au kulizungumzia hawa wazungumzii wake au wapenzi wao, watazungumzia wanawake wengine Ni swala la kisaikolojia, kuepuka ni kuepuka kuwa na mchepuko kwa sababu kiukweli kitendo utamtamani zaidi kuliko mke au mpenzi wako..................sio mim ni ukweli wa sayansi ya saikolojia
nikkwapili
Chiti na demu mkaliiii mpaka demu wako akikufumania nae, badala ya kumpiga mangumi ana mwomba kupiga nae picha, nakumuuliza anatumia mafuta gani, amewezaje kuwa na ngozi nzuri hivyo na namna alivyo tunza shep na kutokua na tumbo kabisa, so akiondoka haondoki na machozi anaondoka na notes alafu akukubali kuwa wewe mbaya, yani ye mwenyewe kabahatisha kuwa na wewe..............ha ha ha naangalia comedi hapa usije ukachukulia serious
Hivi pesa inamaliza matatizo, au matatizo ndio yana maliza pesa??????
Mjadala ni jambo jema na lakujenga....mijadala ya wasanii, wizara, basata itafungua njia ya mafanikio.........tafakari ya mjadala wa jana Kulingana na naibu waziri na basata, kumekosekana mikakati ya kuisaidia sanaa kiuchumi kwa sababu hakuna sera, lakini mbona serikali imekua ikifaidika kiuchumi na sanaa?? Mfano mwaka 2015/16 ukaguzi tu wa filamu na utowaji wa vibali uli iingizia wizara milion 450..... So kwenye kupata mapato hakuitaji sera, ila kusaidia kuna hitaji sera???? Bajeti ya wizara 2015/16 katika bilion 20 ni bilion 3 tu zilitengwa kwa miradi ya maendeleo ya sanaa , hata hivyo ni milion 190 tu ilitolewa yani 6% tu......hapo ikowazi maendeleo ya sanaa ni kiini macho Rasimu ya sera inakaribia kukamilika, kwa upande wa bongo fleva wasanii wengi wanasema hawajashirkishwa Kufungia nyimbo kwa kufuata maadili, wakati wa kampeni 2015 kulikua na nyimbo za matusi tena ya nguoni lakini hazikufungiwa Brazili wanatamba na ile ngoma yao, kigodoro tumefungia Naibu waziri kasema kuna ushirikiano mdogo kati ya basata na wasanii, ndio lazima uwepo maana wasanii wanawaza biashara basata wana ongozwa na sera ya utamaduni hapa interest ni tofauti Tuendelee kujadili, na mijadala hii iwe fursa kwa wasanii, wizara, basata, cosota kujenga zaidi na kupeleka mbele sanaa
Baada ya muda mrefu kua kimya, Jux amerudi na #fimbo link kwenye bio yake. Ni 🔥 Song produced by @Bob_Manecky and @abbah_process video shot by @hanscana_ Enjoy 😉
Katika maisha tafuta nafasi, ukipata nafasi onesha uwezo, ukionesha uwezo kwa bidii utajenga Jina, ukijenga jina utapata fedha na kupiga hatua
Hata uwe na mafanikio kiasi gani, huwezi zuia ndugu zako, watoto au wazazi na wengine unao wapenda, wasipate maradhi, wasi zeeke, wasipate ajali, wasijiskie vibaya, wasiumizwe mioyo,............unapotafuta fedha usisahau kuitafuta Neema ya Mungu maana hayo yote fedha haiwezi kuyaepusha.......bali ni kwa Rehema tu za Mwenyezi
Kuwa mzuri hakuitaji shoping ya Dubai, wigi la malaki, make-up sijui ya saloon gani, wala kamera na maediting..........kuwa mzuri ni kuwa wewe...sunday swagg picha by me
nikkwapili
Watakatifu wabaki nyumbani, wenye dhambi na mapungufu tuelekee kanisani, tukaziponye nafsi zetu, tukamjue Muuumba, kumjua Muumba ni lazima kuijua nyumba ya ibada, maana ndipo wanao mwamini walipo......kanisa la Mungu ni kanisa la jamii sio la mtu binafsi kwa sababu katika Mungu hakuna ubinafsi.......tuikumbuke siku ya bwana na kuitakasa......niwatakie Misa njema.......lakini misa huanza baada ya kutoka kanisani......mana nje ya kanisa ndipo yalipo maudhi, karaa, chuki na hapo ndipo neno la bwana linapoitajika kuongoza matendo na mawazo yetu
Kabla hujaanza kumchunguza mpenzi wako, kwanza jiulize je una roho au moyo wa kuachaaa........kama huna huo moyo basi acha hayo mambo ya kuchunguza wewe sio polisi
Kama unatimiza majukumu yako ya kila siku na unatumia muda wako mwingi kwenye mambo ya msingi, huna haja ya kuwa na hofu juu ya maisha yako ya baadae..................suti by @popula_brand
Duniani kuna makosa ya aina mbili tu, yale ambayo binadamu anaweza kusamehe na asiyo weza kusamehe, kama unataka kudumisha mahusiano, epuka kufanya makosa yasiyo sameeka, hata kama mtu atakwambia amekusamehe kiukweli ni labda amekubali yaishe, au amehepusha shari, au kaamua kuvumilia tu au kumezea. lakini haja samehe, na kuna mambo mengi yatabadilika ndani yake dhidi yako hata kama huoni mabadiliko huenda anayaficha tu.......epuka makosa yasiyo sameeka usidanganywe na neno nimekusamehe sio ukweli wa moyoni
Kama mtoto wa kike analelewa kwa kukatazwa kwenda sehem kibao kibao zaidi ya shule, mara nyingi tuna walea kua nyumbani, kukaa ndani, wakiume wao wanazurura kitaa, wanaenda huku na kule wanajifunza maisha........sasa wasichana nikama wanachorewa mstari ni shuleni na nyumbani, kukaa ndani so tusishangae wanapokuja kuwa wafanyakazi wa kazi za ndani, maana ndio eneo wanalijua vizuri
Mwandishi anasema huna tuna jilinda ki mwili yani mtu asikusukume, asikuzuie njiani kama unapita, asikalie siti yako, asikusachi kwenye mfuko lakini inapokuja swala la mawazo au akili, hatupo makini hatuna taadhari, tunaruhusu mitandao ituamulie nini cha kufikiri, umekaa nyumbani, umekaa na marafiki lakini unatizama mtandaoni unawaza ya huko na kusahau ulio kuwa nao....tawala akili yako, tawala mawazo yako kama unavyo tawala nini uvae, upite njia ipi, usalimiane na nani nakadhalika
Kiraruraruuu

Loading